Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, katika tamko la ofisi ya Ayatollah Sistani imesemwa: “Bibi mtukufu Alawiyya, binti wa Ayatollah Sayyid Mirza Hassan, mjukuu wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Muhammad Hassan Shirazi (Mujaddid Shirazi) – Allah awarehemu wote wawili – na mke wa Marja mkuu Ayatollah Sayyid Ali Husayni Sistani (dama dhilluh), huko Najaf Ashraf ameelekea kwenye rehema za Mwenyezi Mungu.”
Mwili wake mtukufu utaswaliwa na kuzikwa saa 9 asubuhi siku ya Jumatatu, tarehe 6 Rabi’ul-Thani, Msikiti wa Sheikh Tusi.
Vilevile, kikao cha khitma kwa ajili ya kuiombea roho ya marehemu huyo kitaandaliwa siku ya Jumatatu na Jumanne baada ya Swala ya Magharibi na Isha katika Msikiti wa Khadhra.
Maoni yako